28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yaishika pabaya Azam

yangaNA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, ameunda jeshi kamili kwa ajili ya kuiangamiza Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii, utakaochezwa Agosti 22 mwaka huu, katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hiyo inaonyesha kuwa ameanza mikakati ya kuishika pabaya Azam, ambapo ameunda kikosi cha kwanza ambacho anaamini kitaifanyia maangamizi Azam.

Mholanzi huyo, ambaye kikosi chake kimejichimbia Tukuyu, mkoani Mbeya kusaka makali ya kulipa kisasi kwa Azam, aliliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa amefanya mchujo wenye ushindani ili kupata kikosi cha kwanza ambacho ni bora na imara.

Alisema anaamini ametengeneza kikosi cha ushindi na kudai kuwa nguvu nyingi wameelekeza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayoanza Septemba 12, mwaka huu.

“Mashabiki wasiwe na wasiwasi, nimeandaa kikosi imara baada kupima uwezo wa kila mchezaji na kupata wale ambao ninaamini kuwa wakipewa nafasi watafanya kazi kubwa na kufikia malengo yetu,” alisema.

Akizungumzia nyota wapya waliosajiliwa Yanga, Pluijm alisema viwango vyao vinaridhisha, kwani tangu waungane na nyota wengine waliokuwepo ndani ya kikosi hicho wamepata uhuru wa kutosha kuonyesha uwezo wao.

Wachezaji wapya waliosajiliwa Yanga hadi sasa na klabu wanazotoka kwenye mabano ni Deus Kaseke (Mbeya City), Mwinyi Haji na Matheo Simon (KMKM), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Malimi Busungu (Mgambo JKT) na Godfrey Mwashiuya (Kimondo FC).

Nyota wa kigeni waliotua Jangwani ni kiungo mkabaji Thabani Komusoko, mshambuliaji Donald Ngoma na beki Vicent Bossou, raia wa Togo ambaye muda wowote anatarajiwa kusaini mkataba wa kuichezea Yanga.

Wachezaji hao wataungana na nyota wengine wa kigeni waliokuwepo ndani ya kikosi hicho ambao ni kiungo mchezeshaji, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Amissi Tambwe.

Mshambuliaji Mliberia, Kpah Sherman, tayari ameuzwa kwa klabu ya Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini, huku Mbrazil, Andrey Coutinho na Joseph Zuttah ambaye ni raia wa Ghana, wapo katika hatihati ya kubaki kwenye kikosi hicho.

Yanga wakiwa mawindoni Mbeya, tayari wamecheza mechi za kujipima nguvu dhidi ya Kimondo na kushinda mabao 4-1 kabla ya kuvaana na Tanzania Prisons na kuwalaza mabao 2-0.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles