26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Yanga yacheza na hesabu shy

Yanga-leo-72KOCHA wa timu ya Yanga, Hans van Pluijm, amepiga hesabu kali kuelekea mechi mbili zijazo mkoani Shinyanga dhidi ya Mwadui kesho naKagera Sugar mchezo utakaofanyika Jumamosi ijayo.

Mholanzi huyo amesisitiza kuwa pointi sita zote ni muhimu kwake katika mechi hizo, ikizingatiwa yakuwa wanawania kutetea taji lao la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

Pluijm aliliambia MTANZANIA kuwa wanatarajia ugumu kwenye mechi hizo, lakini wamejipanga kupata matokeo mazuri ili kuendeleza kasi yao ya kutetea ubingwa.

“Daima hatudharau mpinzani wetu yeyote, unapofanya hivyo ni hatari sana na imekuwa kawaida sana kuona timu ndogo zikitukamia pale tunapocheza nazo hivyo itakuwa ni mechi ngumu,” alisema.

Pluijm alisema anajua mechi dhidi ya Mwadui itakuwa na upinzani mkubwa hasa kutokana na uwepo wa wachezaji kadhaa waliowahi kuichezea Yanga.

Baadhi ya wachezaji hao ni mshambuliaji Jerryson Tegete, viungo Nizar Khalfan, Razack Khalfan, Athuman Idd ‘Chuji’, Julius Mrope, beki David Luhende, kipa Shaban Kado.

“Najua nakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Azam FC kwenye kuwania ubingwa, hivyo sitakiwi kuacha pointi yoyote katika mechi tunazocheza kwani ili uwe bingwa unahitaji kuwa na pointi nyingi zaidi,” alisema.

Tayari Kocha Mkuu waMwadui, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, ametamba kuiharibia Yanga kwenye mchezo huo kwa kuichapa, kikubwa akijivunia mwenendo mzuri wa kikosi chake hadi sasa wakiwa nafasi ya sita kwa pointi 14.
Yanga yenyewe inajivunia rekodi nzuri iliyokuwa nayo ya kutopoteza mechi hadi sasa ikiwa kileleni kwa pointi 19 sawa na Azam FC katika nafasi ya pili.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwaYanga kuvaana naMwadui tokea ipande daraja msimu huu, ambapo itacheza na Kagera Sugar ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 msimu uliopita kwenye mchezo wa ugenini uliofanyika Uwanja wa Kaitaba.
Bao pekee la Kagera kwenye mchezo huo lilifungwa na mkongwe Paul Ngway kwa kichwa kikali, wakati huo Yanga ikifundishwa na Mbrazil Marcio Maximo huku Kagera ikinolewa na Mganda Jackson Mayanja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles