26.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara yatakiwa kushirikiana na wadau kukuza sekta ya madini

Anna Ruhasha, Geita

Wizara ya Madini imetakiwa kushirikiana na wadau ndani na nje ya nchi katika kutafuta teknolojia za uongezaji thamani wa madini ili kuwezesha ushindani soko la dunia.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba wakati akifunga maonesho ya Nne ya Teknolojia katika sekta ya uwekezaji wa madini mkoani Geita.

Dk. Nchemba amesema kuwa katika kulinda rasilimali zilizopo hasa katika sekta ya madini nikuhakisha zinaongezewa thamani ili kutimiza adhima ya dira ya serika ya uchumi kufika mwaka 2025.

“Nitoe wito kwa wizara ya madini teknolojia inazidi kukua duniani kwa kasi na shirikianene na wadau wa ndani na nje, tukijifungia ndani hatutapata suluhisho na tutachelewesha maendeleo yetu pamoja na kupoteza mali asili tulizonazo kwa kuwa zitakwenda kuwanufaisha watu wengine,” amesema Dk. Nchemba.

Awal,i Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita Saimo Shayo, Geita Gold Mine Limeted (GGML) amesema kampuni kwa miaka Minne kuwa wadhamini wa kuu wa maonesho hayo ni fahari kwa GGML kwa kuwezesha kufua fursa  za biashara na ukuaji kwa sekta ya Madini na Biashara kwa ujumla.

 Aidha , ameongeza kuwa kupitia sheria inayolekeza kutoa fursa kwa  wazawa  GGML kutoka mwaka 2015 imeongeza huduma na bidhaa zinazopatikana nchini kwa asilimia 40 kwa  robo ya mwaka huu, pia GGML imenunua huduma kutoka Tanzania na bidhaa zinazopindukia zenye thamani ya Dola milioni 90.

Wakati huo huo ameongeka kuwa ndani ya mwaka moja wamewafikia zaidi ya wafanyabishara zaidi 300 mkoani Geita na kuwapa mafunzo wezeshi na Kati yao wemeweza kupata tenda za kufanya kazi mgodi mafuta na Chemical zenye thamani dola nane mpaka 10.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amesema mkoa huo kupitia kauli mbiu ya mkoa wa Geita, inayosema Geita ya dhahabu utajiri na heshima inaleta mabadiliko kwa wakazi wa mkoa huo, kujiari au kuajiriwa na kujiongzea mapato kutoka na fursa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles