27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Kilimo yaja na mwarobaini wa uhaba wa sukari

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Uzalishaji wa sukari nchini umetajwa kongezeka katika kipindi cha miaka mitano kutoka tani 295,775 mwaka 2015/2016 hadi tani 377,527 zinazotarajia kuzalishwa msimu wa 2020/2021.

Hayo yamebainishwa leo Januari 27, jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo. Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali ya uzalishaji wa sukari hapa nchini.

Amesema mafanikio hayo ya kuongezeka kwa uzalishaji ni matokeo ya utekelezaji wa sera na mikakati ambayo serikali imeweka kuhakikisha wazalishaji wana mazingira mazuri ya kufanya upanuzi wa mashamba na wakulima kuongeza tija.

Aidha, katika msimu wa mwaka 2020/2021 jumla ya tani 377,527 za sukari zinatarajiwa kuzalishwa kutoka kwenye viwanda vilivyopo nchini vikiwemo Kilombero Sugar Company Ltd, Mtibwa Sugar Estate, Kagera Sugar Ltd, TPC Ltd na Manyara Sugar Ltd.

“Kwa hapa nchini mahitaji ya sukari kwa ujumla kwa matumizi ya kawaida na viwandani ni tani 655,000 kwa mwaka, hivyo ili kuongeza uzalishaji serikali imejipanga kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima wadogo.

“Lakini pia tunataka kuona viwanda vikiongeza uwezo wa kuchakata miwa inayozalishwa na kuongeza tija kwa uwepo wa mbegu bora na viuatilifu,” amesema Prof. Mkenda.

Amesema kutokana na uhaba wa sukari uliopo na miwa ya wakulima kubaki mashambani bila kuvunwa kwa sababu ya ufanisi na uwezo mdogo wa viwanda, serikali imeelekeza kiwanda cha Kilombero na viwanda vingine kuongeza na kuimarisha uwezo wa uchakataji wa miwa.

“Lengo ni kunusuru hasara kubwa wanayoipata wakulima kwa kutovuniwa miwa yao na kupelekwa kuchakatwa viwandani.

“Serikali haitosita kuchukua hatua ya kuruhusu mwekezaji mwingine kujenga kiwanda cha kati kimoja au viwanda vidogo viwili endapo mwekezaji aliyopo sasa katika bonde la Kilombero atashindwa kufanya upanuzi unaostahili kwa wakati ili miwa ya wakulima wadogo takribani tani 200,000 inayobaki katika bonde la kilombero ipate soko la uhakika,” amesema Prof. Mkenda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles