25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wizara ya Kilimo kutenga bajeti, kuanzisha kitengo cha kilimo hai

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema serikali itaanzisha kitengo cha kinachoshughulika na masuala ya kilimo hai katika wizara yake na kukitengea bajeti.

Aidha, amesema itaanzisha benki kubwa ya mbegu za asili kabla ya kuanzisha mfumo wa kusafisha mbegu hizo na kuzirudisha shambani.

Bashe amesema hayo leo Alhamisi Oktoba 21 jijini Dodoma katika Kongamano la Pili la Kitaifa la Kilimo Hai linaoendelea jijini Dodoma leo na kesho.

Amesema katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23 wizara yake itatenga bajeti kwa ajili ya kilimo hai kutokana na umuhimu wake kwani magonjwa mengi yanatokana na aina ya vyakula watu wanavyokula.

“Pamoja na mambo mengine tutaweka kitengo ndani ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), kitakachofanya utafiti wa kilimo hai.

“Mbegu za asili zikisafishwa vizuri mkulima akazitumia matokeo yake yatakuwa mazuri mno. Lakini pia mazao ya kilimo hai kwenye soko yanapata bei nzuri kuliko mengine,” amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, DK. Soud Nahodha Hassan, amesema kwa upande wa Zanzibar asilimia 60 ya jilimo kinachofanyika visiwani humo ni kilimo hai.

“Na sisi wizara tunajipanga kwa mwaka wa fedha tutaiweka bajeti ya kuendekeza kilo hai Zanzibar kwa sababu tunaona umuhimu wake, nimefarijika pia kuona huku bara napo watu wanakitaka kilimo hai,” amesema Dk. Soud.

Kongamano la Pili la Kitaifa la Kilimo Hai, kinafanyuka jijini Dodoma kwa siku mbili leo na kesho ambapo limeshirikisha wadau mbalimbali wakiwamo Mkulima Mbunifu, Shamba la Kioganiki Kwanyange na wengine wameshiriki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles