Wimbo wa Adele wavunja rekodi You Tube

0
672

2011 MTV Video Music Awards - ShowLAS VEGAS, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Adele Adkins, amevunja rekodi nyingine ya wimbo wake wa ‘Hello’ ambapo video ya wimbo huo tayari umefikisha idadi ya watu bilioni 1 walioutazama kupitia You Tube.

Video hiyo tangu imeachiwa hadi sasa imefikisha siku 87, ikiwa ni tofauti na siku 158 ambazo wimbo wa Park hangul ‘Psy’ wa ‘Gangnam Style’ uliweka rekodi ya kutazamwa na idadi kubwa ya watu.

Mtandao wa You Tube umeweka wazi kwamba, Adele kwa sasa anashikilia rekodi hiyo kwa kuivunja ile ya nyota raia wa Korea Kusini.

“Kama kuna mtu anatakiwa kupewa sifa kwa kufanya vizuri kwenye You Tube, basi Adele anastahili sifa hiyo kwa kumpiku mwenzake kutoka Korea Kusini,” alisema Susanne Daniels Mkurugenzi wa You Tube.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here