23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Will Smith: Nitakuja kuwa rais wa Marekani

Will SmithNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki na filamu nchini Marekani, Will Smith, amesema bado ana ndoto za kuja kuwa rais wa nchi hiyo kwa miaka ijayo.

Msanii huyo ambaye anafanya vizuri katika filamu, ameamua kurudi tena kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa miaka mingi, lakini mbali na kufanya muziki amesema kuwa lengo lake ni kuja kuwa rais wa Marekani.

“Ninaamini kila kitu kinawezekana, lakini kwa upande wangu ni kwamba siku moja nije kuwa rais wa Marekani, hii ni mipango yangu kwa kuwa ninaamini ninaweza kuiongoza nchi.

“Wazo la kuja kuwa rais lilikuja baada ya kufanya mazungumzo na Donald Trump, ambaye amenishawishi kwa asilimia kubwa kwa kuniambia kwamba hakuna kisichowezekana duniani kama una nia nacho, hiyo ni kauli ambayo inanitia moyo kwa kiasi kikubwa,” alisema Smith.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles