24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

WHC yakumbushwa kuwakumbuka Walimu

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Kampuni ya Nyumba ya Watumishi Housing (WHC) imekumbushwa kujenga nyumba kwa ajili ya walimu kwani wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya makazi hatua inayosababisha baadhi kukimbilia mijini.

Wito huo umetolewa Jumatatu Juni 28, 2021 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohammed Mchengerwa akizungumza na Watumishi wa Watumishi Housing Company (WHC).

Nyumba za Watumishi Housing zilizoko Bunju.

 “Watumishi tusijiweke kibiashara zaidi kwani tutashindwa kusaidia watumishi wetu ambao ndio lengo mama la kuanzishwa kwa WHC, hivyo pamoja na mambo haya tuwakumbuke walimu.

“Kwa hiyo nilazima tujipange ili tuweze kujiendeshe lakini pia tujipange ili, tuangalie uwezekano wa kupunguza kabisa au kumaliza kero ya nyumba za walimu wetu, kwa hiyo andaeni mpango kwani yapo maeneo ambayo tunawapeleka walimu lakini wanashindwa kwenda saabu hawana mahala pa kukaa.

“Kwa hiyo muone namna gani mtaweza kukabiliana na hilo kwa walimu wetu kote nchini ili kurahisisha walimu kubaki kwenye maeneo wanayopangiwa,” amesema Mchengerwa.

Amewataka WHC kwenda kwenye maeneo ya ndani zaidi ambako kumekuwa na changamoto ya kufikiwa na walimu wengi sababu ya makazi.

“Lazima tukumbuke kwamba rais ndiye mfariji namba moja ndiyo maana mpaka kufikia jana (Juzi) saa nane Mchana Rais Samia Suluhu amepokea na kuridhia upandishwaji wa madaraja ya watumishi wa umma zaidi ya 116,000.

“Hivyo hiyo ina maana kwamba mishahara ya watu wengi imepanda, kwani ofisi yangu ilimuomba zaidi ya Sh bilioni 300 ambazo amezitoa hivyo ni lazima nasi tuhakikishe kuwa tunafanya sehemu yetu kwenye kuboresha makazi ya walimu,” amesema Mchengerwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing, Dk. Fred Msemwa amesema ofisi yake itatekeleza maelekezo ya Mchengerwa kwa kuongeza ubunifu ili kujenga nyumba za gharama nafuu kwa watumishi kwenye majiji na maeneo yenye uhaba wa nyumba hususani vijijini na kwenye maeneo yenye huduma za shule na afya.

Dk. Msemwa ameahidi kuwa, ofisi yake itaendelea kubuni miradi itakayowahakikishia Watumishi wa Umma pamoja na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii upatikanaji wa nyumba za gharama nafuu kwa kuzingatia kipato chao.

Aidha, amemshukuru Mchengerwa kwa kuipongeza ofisi yake kwa ubunifu wa miradi ya nyumba ambazo zimewawezesha Watumishi wa Umma katika maeneo yenye miradi ya nyumba za Watumishi Housing kupata nyumba za kupanga na kuishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles