Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Chakula Duniani, WFP David Beasley ametaka kuongezwa fedha zaidi zitakazonunua vyakula vya kutosha ili kusaidia mamia ya watoto wanaokufa kwa njaa duniani.
Amesema nchi nne zilizoathirika zaidi ni Yemen, Sudan Kusini, Somalia na Nigeria, na kuna uwezekano watoto mia sita wakafariki ndani ya miezi minne ijayo kwa kukosa chakula.
Ameitaka pia Saudi Arabia kuisaidia Yemen kukabiliana na baa kubwa la njaa linaloikabili.
Pamoja na mambo mengine, vita inatajwa kuwa sababu kubwa ya watoto kukosa chakula katika sehemu zenye migogoro.