27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wenyeji Brazil watolewa kwenye Olimpiki

3971

RIO DE JANEIRO, BRAZIL

WENYEJI wa michuano ya Olimpiki, Brazil, tayari wameyaaga mashindano hayo kwa upande wa timu ya taifa ya mpira wa miguu.

Timu hiyo ya wanawake ilikuwa na ndoto ya kufanya vizuri kwenye viwanja vya nyumbani na kutwaa medali za dhahabu, lakini ndoto hizo zimefutwa baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-3 ya mikwaju ya penalti dhidi ya wapinzani wao kutoka nchini Sweden.

Mchezo huo wa nusu fainali uliopigwa usiku wa kuamkia jana, ulimalizika dakika 90, huku timu hizo zikiwa hazijafungana, hivyo waliongeza dakika 30 lakini hakupatikana mbabe ndipo wakaenda kwenye matuta.

Hata hivyo, timu hizo zilipokutana katika hatua ya awali, Brazil ilifanikiwa kushinda mabao 5-1 hatua ya makundi, hivyo Brazil waliamini kuwa watapata nafasi ya kufika fainali, lakini ndoto hizo zimefikia mwisho.

Kocha wa timu ya taifa ya Sweden, Pelle Olsson, anaamini ana nafasi ya kuwa bingwa katika michuano hiyo baada ya kufanya vizuri akiwa na timu ya taifa ya United States na kutwaa medali za dhahabu mwaka 2008 na 2012, na sasa anaamini ana nafasi ya kuendeleza ubabe huo huku akiwa na timu hiyo.

Timu hiyo inatarajia kukutana na Ujerumani katika mchezo wa fainali, huku Ujerumani ikiingia kwenye hatua hiyo baada ya kuichapa Canada mabao 2-0 kwenye hatua ya nusu fainali, wakati huo Brazil wakitarajia kucheza na Canada kumtafuta mshindi wa tatu ambaye atapata medali ya shaba.

Hata hivyo, katika soka la wanawake Brazil haijawahi kupata medali ya dhahabu, hivyo mwaka huu walikuwa na uhakika wa kuipata, wakati huo kwa upande wa Sweden, hii itakuwa ni fainali yao ya kwanza tangu mwaka 1948, ambapo timu ya taifa kwa upande wa wanaume ilifanikiwa kutwaa medali ya dhahabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles