NA KULWA MZEE-DODOMA
SERIKALI imetangaza kuwanyang’anya umiliki wa ardhi watu wenye uraia wa nchi mbili na imeondoa tozo kubwa ya asilimia 67 iliyokuwa ikiwakwaza Watanzania na wawekezaji katika umiliki wa ardhi.
Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alipokuwa akichangia na kujibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge,
Lukuvi alisema baada ya kuondoa tozo hiyo, kodi mpya itaanza kutumika Julai mwaka huu. Kwamba kama kuna mtu alikuwa anatakiwa kulipa Sh milioni 100 sasa atalipa Sh milioni 33, lengo likiwa ni kuwapa nafuu Watanzania wote waweze kumiliki ardhi na Serikali kupata mapato.
Alisema wawekezaji walikuwa hawawezi kufika Dodoma kwa sababu ya mkanganyiko wa umilikaji wa ardhi.
“Sasa hivi wenye hati za kumilii ardhi kwa miaka 33 wataendelea kupata hati za miaka 99 kama ilivyo kwa watu wengine nchini,” alisema.