24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

WENGER KUPUNGUZA WACHEZAJI

 

 

LONDON, England

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amikiri kuwa na mpango wa kupunguza baadhi ya wachezaji katika kikosi chake kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Klabu hiyo imejikuta ikitumia muda mwingi kusajili dirisha la usajili na kuzima fununu za kuuza wachezaji wake kama Alexis Sanchez na Olivier Giroud.

Arsenal imewasajili wachezaji kama Alexandre Lacazette na Sead Kolasinac, ambao wameifanya klabu hiyo kuwa na matumaini makubwa msimu mpya.

Usajili huo pamoja na wachezaji waliopo ndani ya kikosi cha Wenger, unatarajiwa kuhamasisha hali ya ushindani, hata hivyo, kocha huyo anataka kuwapunguza baadhi ya wachezaji ili kuweka uwiano sawa katika ushindani.

“Niwe mkweli, idadi ya wachezaji ni kubwa mno,” alisema kocha huyo, baada ya kunyakua kombe la Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea.

“Tutawaacha wachezaji wengine wataondoka, ushindani katika kikosi ni afya, lakini hautaweza kuwa ushindani kama kukiwa na wachezaji kupita kiasi,” alisema Wenger.

Arsenal tayari imewaachia wachezaji wake chipukizi kama Wojciech Szczesny, Yaya Sanogo na Emiliano Martinez, ambao wamejiunga na klabu nyingine.

Mshambuliaji wa Kihispania, Lucas Perez, anaweza kuwa mmoja kati ya wanaotakiwa kuondoka katika timu hiyo, baada ya kukaa miezi 12 tangu asajiliwe akitokea klabu ya Deportivo La Coruna.

Arsenal pia wanaweza kumruhusu Sanchez au Giroud kuondoka katika kikosi chao na kuunda kikosi watakachoamini kinaweza kuleta mafanikio katika msimu mpya.

Beki wa timu hiyo, Mohamed Elneny, alisema lengo la benchi la ufundi la timu hiyo ni kuhakikisha kikosi hicho kinakuwa katika ubora na uimara thabiti ili kukisaidia kunyakua mataji.

“Klabu inataka kutuweka pamoja kwa kuimarisha hali ya kikosi, hata kwenye kipindi kigumu.

“Kuna hali ya kukata tamaa katika msimu, hivyo ni jukumu la benchi la ufundi kuhakikisha tunapita salama katika kipindi hicho,” alisema Elneny.

Timu ya Arsenal itafungua msimu mpya wa Ligi Kuu England Ijumaa kwa kucheza dhidi ya Leicester City.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles