24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger hana mpango wa kustaafu

arsene-wenger_2645586bLONDON, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amesisitiza kuwa mpaka sasa hajapanga tarehe rasmi ya kustaafu kufundisha soka.

Wenger amesema bado anaamini anaweza kufanya makubwa kwa klabu ya Arsenal hasa msimu huu wa Ligi Kuu nchini England huku akiwa na matumaini makubwa ya kuchukua ubingwa.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65, amekuwa na furaha ya kufikisha miaka 19 ya kuifundisha klabu ya Arsenal, hata hivyo mashabiki wa klabu hiyo walianza kumchoka kutokana na maendeleo mabaya ya timu.

“Bado sijafanya maamuzi ya kupanga tarehe ya kustaafu lakini siku zote naogopa kupanga siku maalumu ila ninaamini itafika nikipanga mwenyewe.

“Kuna makocha wenzangu huwa wanatangaza kuwa mwakani wanastaafu, lakini mwaka ukifika utasikia wanahama timu na wanaendelea na kazi yao. Lakini kwa upande wangu nikisema nastaafu basi nitastaafu kweli,” alisema Wenger.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles