29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wazungu kushuhudia mavitu ya Mgosi

Winfrida Mtoi, Dar Es Salaam

WACHEZAJI wa timu ya St. Pauli ya nchini Ujerumani, wanatarajia kushuhudia mchezo wa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, kati ya Simba Queens na TSC utakaochezwa leo, Uwanja wa Simba Mo Arena jijini Dar es Salaam.

Wajerumani hao wapo nchini kwa ziara maalumu ya kimichezo huku wenyeji wao wakiwa  Simba Queens, ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano wa timu hizo mbili.

Ikumbukwe kwamba, Simba Queens ilifanya ziara ya kimichezo nchini Ujerumani mwaka jana na St Pauli ndio walikuwa wenyeji wao.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’, alisema  wageni wao watakuwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

Alisema wamekuwa nao muda wote tangu walipotua nchini wiki iliyopita, wakifanya mazoezi pamoja kabla ya kucheza mechi ya kirafiki.

“Tutacheza mechi za kirafiki na wageni wetu timu ya St. Pauli, lakini hadi tumalize mechi ya Ligi Kuu kesho (leo) na watakuwa uwanjani wakituangalia,”  alisema Mgosi.

Mgosi alisema wameelekeza nguvu nyingi katika michezo ya Ligi kwa sababu lengo lao ni kuchukua ubingwa wa michuano hiyo.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Simba Queens na pointi 26 baada ya kucheza mechi 10, imeshinda nane na sare mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles