Taylor Swift alitikisa mwaka 2019

0
593

New York, Marekani

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Taylor Swift, ametajwa kuwa msanii namba moja ambaye alifanya mauzo makubwa ya muziki kwa mwaka 2019.

Kwa mujibu wa mtandao wa IFPI, Jumatatu wiki hii walitoa orodha ya wasanii duniani ambao walitikisa sokoni kwa mwaka huo na msanii huyo akashika namba moja.

Mwaka 2019 msanii huyo aliachia albamu inayojulikana kwa jina la Lover na kumfanya ashinde kuwa msanii bora wa mwaka huo kwa mara ya pili, huku mara ya kwanza ikiwa mwaka 2014 ambapo aliachia albamu inayojulikana kwa jina la 1989.

Albamu ya Love iliachiwa tangu Agosti mwaka jana na kuuza jumla ya kopi milioni 3 ndani ya wiki moja ya kwanza nchini Marekani. Wasanii wengine ambao walifanya vizuri ni pamoja na Ed Sheeran akishika nafasi ya pili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here