28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

… Waziri wa JK adaiwa kuiba ripoti ya CAG

Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete

Na Bakari Kimwanga, Dodoma

JOTO la kashfa ya wizi wa Sh bilioni 306 katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), limeendelea kupanda mjini Dodoma, huku  mmoja wa mawaziri waandamizi akidaiwa kuuiba ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kunyofoa baadhi ya kurasa kisha kuzisambaza mitaani.

Tangu kuwasilishwa kwa ripoti ya CAG bungeni wiki iliyopita, kumeibuka makundi mawili yanayokinzana moja likitaka iwasilishwe na jingine likipinga.

Chanzo cha habari cha kuaminika kililiambia MTANZANIA mjini Dodoma jana  kuwa, baada ya kuibuliwa madai ya kuibiwa kwa nyaraka hizo katika  ofisi ya Katibu wa Bunge na kunyofolewa baadhi ya kurasa makundi hayo yameshutumiana juu ya wizi huo.

Kutokana na hali hiyo, waziri huyo (jina tunalo), ametajwa kuwa ndiye aliyeiba ripoti hiyo na kuanza kuisambaza.

“Tangu ilipowasilishwa ripoti ya CAG pamoja na ile ya Takukuru hapa Dodoma hali si shwari, maana kati yetu wabunge hasa wa CCM tumekuwa hatuaminiani tena… na sasa waziri huyu ndiye amekuwa akitajwa kusuka mikakati ya kuiba ripoti ya uchunguzi katika Ofisi ya Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila.

“Lakini hili halisaidii ni lazima ripoti isomwe na wezi waliokula fedha hii ya walipa kodi wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria kama ilivyo kwa wezi wengine,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutoandikwa gazetini.

Kamanda wa Polisi

Akizungumzia tukio hilo jana mjini hapa,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema hadi sasa jeshi lake linawashikilia vijana wawili ambao wanadaiwa kusambaza nyaraka hizo zilizoibwa katika Ofisi ya Katibu wa Bunge.

“Jana (juzi),tulipata taarifa kutoka kwa Katibu wa Bunge kuwa kuna watu wanasambaza nyaraka kutoka Ofisi ya Katibu wa Bunge,baada ya taarifa hiyo tulianza msako na kufanikiwa kuwakamata vijana wawili.

“Mmoja wa vijana wale tulimkuta akiwa na nyaraka tatu ambazo mbili zilikuwa na muhuri wa ofisi ya Katibu wa Bunge tulikwenda hadi katika hoteli aliyofikia na kufanya uchunguzi na tulipombana zaidi alikiri kupewa na mbunge mmoja ambaye kwa sasa jina lake tunalihifadhi kwa sababu ya uchunguzi.

“Hatua tunayofanya sasa ni kuzipeleka karatasi hizi kwa mtaalamu wa maandishi kwa uchunguzi wa zaidi na swali la kujiuliza kama zilikuwa za siri je huyu kijana alizipataje na kuanza kuzisambaza mitaani?,” alisema na kuhoji Kamanda Misime.

Juzi Kambi Rasmi ya Upinzani, iliibuka na kutoa taarifa za kugazaa nyaraka hiyo ya CAG ambayo bado infanyiwa kazi ya kiuchunguzi na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema ripoti iliyonaswa ikizagaa mitaani ni ile iliyokabishi kwa CAG kwa Katibu wa Bunge.

Mbali na hilo alidai  ripoti hiyo imenyofolewa baadhi ya kurasa kwa lengo la kupotosha ukweli kwa umma kutokana na uzito wa suala hilo.

“Kurasa ya 57, 58 na 59 zimenyofolewa na kundi la maharamia ambao wamepiga kambi hapa Dodoma kwa ufadhili wa kigogo mmoja kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

“Mkakati wao ili ionekane kuwa ripoti haifai kuingizwa bungeni kutokana na kile wanachotaka kudai kuwa imeshatoka mbele ya umma na si siri tena kwa hili hatukubali hata kidogo na tunataka Jumatatu iingie bungeni.

“Asubuhi Jumatatu (leo), tutakutana wabunge wote wa Kambi Rasmi ya Upinzani na kutoka na azimio ambalo tutaliwasilisha bungeni kuhusu suala hili,” alisema Mbatia.

- Advertisement -

Related Articles

3 COMMENTS

  1. CCM SASA YAMETIMIA maana tulipikuwa tunaikosoa CCM hawakukubai, walisema tunachuki binafsi na ccm. Sasa yanayotkea ni nini kama wangesikia ushauri leo wangejirekebisha. Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu, leo ccm imevunjika guu, na huundiyio mewisho wa ccm, je nani atakuja kuichagua ccm labda wapenda kanga, pilau, wajinga wasioujua kinachoendelea. CCM haifai kwani imekuwa ni janga la taifa, ccm ni maafa kwa watanzania Ndiyo kwa maana wiki jana niliandika kwamba “Katiba haramu ya ccm ni kitanzi chamauti ya wananchi wa Tanzani”, wengine walibeza na kudharau, sasa leo yako wapi? Utake usitake, ukweli lazima ujitenge na uwongo, na ukwel utakuweka huru. CCM imejifanyika kampeni ya kujizika, tunasubiri mazishi makubwa mwakani. Atakayeichagua ccm ni zuzu kama wanavyosema wabongo ni kweli, nchi sasa tuwape Upinzani (Ukawa nao wajaribu) hawa wameiba mapaka wakajiiba wenyewe. Mwulize mwenzako uliye naye karibu” JE MWAKANI UTACHAGUA CHAMA GANI? Atakayechagua ccm ni yule antaka kuungana na shetani anayeleta mauaji. je, kama una akili safi unaweza kuchaguakifo?

  2. hebu tuwe kama wachina,nafikiri ndio njia pekee ya kupata maendeleo’bila hivyo hatuwezi kufika,ila naamini watu wakichoka na tabia hii wao ndio waamuzi wa mwisho ;ila bado najipa faraja kwamba yote yataisha siku moja !

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles