33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa Fedha Afrika Kusini ajiuzulu

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

WAZIRI wa Nhlanhla Nene amejiuzulu wadhifa wake baada ya kukubali kuwa aliwahi kukutana na familia ya Gupta ambayo inakabiliwa na mashtaka ya rushwa.

Familia ya Gupta ambayo ni ya wafanyabiashara imekuwa ikituhumiwa kuwa na ukaribu usio wa kawaida na Rais wa zamani, Jacob Zuma wakidaiwa kushirikiana katika kughushi mikataba ya Serikali na kuwa na ushawishi katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

Ushawishi huo wa kina Gupta ulitafsiriwa kama ‘kutekwa nyara’ kwa Serikali ya Rais Zuma ingawa pande hizo mbili zilikuwa zikiyakana madai hayo.

Kwa kujiuzulu huko nafasi yake imechukuliwa na Gavana wa zamani wa Benki Kuu, Tito Mboweni.

Hii ni mara ya tano tangu mwaka 2014 kwa Afrika Kusini kubadili Waziri wa Fedha.

Wiki iliyopita Nene aliiambia tume ya uchunguzi wa sakata la akina Gupta ijulikanayo kama Tume ya Zondo kuwa aliwahi kuhudhuria kikao na wafanyabiashara hao ingawa awali alikataa kukutana na watu hao.

Kabla ya kutangaza kujiuzulu, waziri huyo alisema hakuna mapendekezo aliyoyatoa ambayo yako kinyume na sheria wakati alipokutana na wafanyabiashara hao akiwa anahudumu katika Serikali ya Zuma, lakini anakiri kulikuwa na msukumo wa kisiasa ambao umemfanya kuchukua uamuzi huo.

Nene alifukuzwa kazi na Rais Zuma mwaka 2015 ikiaminika ni kutokana na ushawishi wa kina Gupta, lakini Februari mwaka huu alirudishwa katika wadhifa huo na Rais Cyril Ramaphosa.

Katika hotuba yake wakati anakubali kujiuzulu kwa Nene, Rais Ramaphosa alisisitiza sababu ya kulinda masilahi ya uongozi wa fedha na Serikali, ingawa kukubali kwake kwa waziri huyo kujiuzulu kunaleta hofu ya kuondoa imani ya watu katika Serikali yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles