24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI UMMY AMLILIA BINTI ALIYEKUWA NA UVIMBE BEGANI

Na Mwandishi wetu –


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema amesikitishwa na kifo cha msichana Marim Sandalu (17) aliyekuwa na uvimbe begani.

Mariam ambaye ni mkazi wa Masasi mkoani Mtwara, amefariki dunia leo alfajiri akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI).

Akizungumza na Mtanzania Digital, Waziri Ummy amesema inasikitisha kwani msaada wa Watanzania haukuweza kuokoa maisha yake.

“Tutaongeza jitihada zaidi kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwahi hospitalini kufanyiwa uchunguzi na kuzingatia maelekezo ya madaktari wanayopewa ikiwamo kuanza matibabu mara moja na si kwenda kukaa nyumbani na mgonjwa,” amesema Waziri Ummy ambaye hivi karibuni alimtembelea Mariam hospitalini kumjulia hali.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Watanzania kwa awamu ya tano wamezidi kujihusisha na siasa mbovu. Kila siku ni siasa, kuhama watu, kumuunga mkono raisi, kumsifu raisi, huku mambo muhimu ya kijamii ambayo serikali inabidi itoee elimu mbadala kwa Wananchi ni zero. Wananchi wanalazimika kuuingia chama, kushika dola, kupigia makofi hata pasipo husika. Huyu binti alipelekwa hospitali huko kwao. Je majukumu ya madactari ni nini. Yanamwachia mzigo mzazi asiyejua mbele wala nyuma na kazidiwa na majukumu.Mnawalaumu jamii wasiofunguka namna gani wapaze sauti zao wakati wameshazipaza kwa kumpeleka mtoto hospitali. Taaluma kama za afya inabidi zishirikiane na kusambaza matatizo kama haya Muhimbili na yatatuliwe mara moja bila kujali cheo cha mtu. Utakuta ni viongozi wa juu tu ndio wanaochukuliwa maanani.Usawa Tanzania haupo. Na hili linazungumziwa tu midomoni mwa vigogo wengi bila kutekelza. Inakuwa wimbo mmoja baada ya mwingine, huku wakifaidi mishahara minono na shamrashamra nyingi tu. ubwana na utwana wa nchi hii ni tatizo kubwa sana na ndilo linalowafanya watanzania wengi wasomi kukimbilia kwenye siasa. ubunifu kimaendeleo zero.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles