25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Simbachawene, “awapongeza Walimu Mpwapwa”

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amewapongeza Idara ya Elimu Sekondari ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwa kufanya vizuri katika Mtihani wa kidato cha nne ambapo imeshika nafasi ya kwanza kimkoa na matokeo ya kidato cha pili ambapo imeshika nafasi ya pili kimkoa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, George Fuime (kushoto) akiwa na Maafisa Elimu na Walimu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa wakifuatilia kikao cha Bunge, wakati wa Bunge la 12 Mkutano wa 14 unaoendelea jijini Dodoma.

Kauli hiyo ameitoa alipokutana na Ujumbe huo bungeni leo Februari 7, 2024 jijini Dodoma, ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, George Fuime na Afisa Elimu Sekondari pamoja na Maafisa elimu na walimu wakuu wa sekondari 32 za Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.

Amesema kila jambo linalotokea lina msingi wake na msingi mkuu ni utendaji mzuri wa ushirikiano katika kazi kwa kuangalia mazuri ya kila kitu na mazuri ya kila mtu.

“Kuangalia mazuri ya wanafunzi mazuri ya walimu na mazuri ya viongozi yanasaidia katika kuweza kupata matokeo mazuri,” alisema Simbachawene.

Kwa upande wake Afisa elimu sekondari Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mwalimu Bernadetha Thomas amesema waziri amewaalika baada ya kufanya vizuri matokeo ya kidato cha nne.

“Tumepanda kutoka asilimia 88 kiwango cha mwaka juzi mpaka asilimia 95 kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la kwanza mpaka daraja la nne kwa mwaka 2023 na mchango huu umechangiwa na shule 11 za kata,” amesema Bernadetha na kuongeza kuwa:

“Tumechukua ushauri wa waziri kama maelekezo kwetu kwa kuwa amekuwa akituongoza katika mabadiliko chanya katika sekta ya elimu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles