ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa Afghanistan, Amrullah Saleh, amesema hautambui utawala wa Taliban na hana mpango wa kujisalimisha baada ya kukimbia mjini Kabul.
Saleh alikimbia Kabul mwezi huu mara tu Taliban walipouteka Mji huo, lakini amebaki Afghanistan, tofauti na Rais Ashraf Ghani aliyekimbilia Umoja wa Falme za Kiarabu.
Baada ya Rais Ghani kuondoka, Saleh aliyewahi kuwa Makamu wa Rais, alitangaza kuwa yeye ndiye atakayeiongoza nchi hiyo na atahakikisha Taliban wanajutia.
Katika hotuba yake, Saleh alimtupia dongo aliyekuwa bosi wake, Rais Ghani, akisema amekuwa mnafiki kwa hatua yake ya kukimbia nchi.