25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waziri Mkuu Gabon afariki dunia

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Gabon, Casimir Oye Mba, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79, chanzo kikiwa ni ugonjwa wa Corona.

Taarifa za kifo cha kiongozi huyo zimethibitishwa na familia yake  kuwa alikuwa akiendelea na matibabu nchini Ufaransa baada ya wiki moja mjini Libreville, Gabon.

Rais wa Gabon, Ali Bongo, ametuma salamu za rambirambi kwa Oye Mba aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo kuanzia mwaka 1990 hadi 1994.

“Nimesikitika kusikia asubuhi ya leo (jana) juu ya kifo cha Casimir Oye Mba. Nitamkumbuka mtumishi aliyejitoa kwa ajili ya watu,” ameandika Rais Bongo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles