Tigray, Ethiopia
Waziri Mkuu nchini Ethiopia Abiy Ahmed amesema kuwa hatakubali uchaguzi mkuu uliocheleweshwa kutumiwa kwa maslahi ya mataifa ya nje.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Shirika la Habari la Ethiopia (ENA) linalomilikiwa na serikali liliripoti kuwa Uchaguzi huo utaamuliwa na Ethiopia na raia wake tu, sio kutimiza maslahi ya watu wa nje.
Pia waziri Abiy alishutumu nchi ambazo hakuzitaja jina kwa kufanya kampeni dhidi ya Ethiopia wakati akifanya uzinduzi wa eneo la viwanda katika Mkoa wa Afar.
“Nchi zilizo na uchumi imara au vyombo vingine viko katika kampeni dhidi ya Ethiopia na lengo likiwa kuamua jinsi Waethiopia wanapaswa kuishi,” amesema waziri Abiy.
Ethiopia imekuwa chini ya shinikizo kutoka kwa Marekani na Jumuiya ya Ulaya juu ya madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na mzozo wa kibinadamu kaskazini mwa mkoa wa Tigray.