23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Kesi ya aliyekuwa Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma yasongezwa Mbele

Cape Town, Afrika Kusini

Kesi ya ufisadi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma imesogezwa mbele hadi 26 Mei ambapo ombi rasmi litawasilishwa.

Wafuasi wa Jacob Zuma walikusanyika nje ya Mahakama Kuu ya Pietermaritzburg kabla yeye kujitokeza.

Rais huyo wa zamani anakabiliwa na makosa 16 ya ufisadi unaohusiana na makubaliano ya silaha ya mabilioni ya dola ikiwa Jumla ya mashahidi 217 wanatarajiwa kutoa ushahidi dhidi yake.

Kesi hiyo inahusu makubaliano ya biashara ya silaha na kampuni ya silaha ya Ufaransa Thales ambayo ilikuwa na nia ya kuboresha ulinzi wa Afrika Kusini mwishoni mwa miaka ya 1990.

Jacob Zuma na kampuni hiyo wamekana mashtaka ambayo ni pamoja na udanganyifu, ulaghai na uhujumu uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles