24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA MILIONI 10/-

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa msaada wa Sh milioni 10 kumuwezesha Ernest Masenga kutatua changamoto zinazomkabili.

Masenga  alikuwa msanii wa muziki wa dansi na hivi  sasa anasumbuliwa na maradhi ya miguu. Pia makazi anayoishi si salama na yanahitaji kukarabatiwa.

Majaliwa alitoa msaada huo   Dares Salaam jana baada ya kuguswa na hali ya maisha ya msanii huyo aliyemuona kupitia kipindi maalumu kilichoonyeshwa na TBC Sepemba 5,  mwaka huu. Kipindi hicho kiliongozwa na  Godfrey Nago.

“Nawaomba Watanzania wenzangu tumsaidie mwezetu aweze kuishi vizuri kwa sababu sanaa yake imesaidia   kuelimisha na kuburudisha umma,” alisema Majaliwa

Nago ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya Masenga, alisema atahakikisha anasimamia vizuri fedha hizo zitumike kama ilivyokusudiwa.

Alimshukuru Waziri Mkuu kwa kuwaunga mkono na kutoa msaada huo kwa sababu ameonyesha Serikali inawajali wananchi wake na TBC itaendelea kuwaomba wadau mbalimbali wajitokeze  kumsaidia msanii huyo.

Mjomba wa msanii huyo, Kanuti Mloka ambaye aliiwakilisha familia, alimshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo.

Alisema  familia imeshindwa kumsaidia Masenga kutokana na hali duni ya maisha waliyonayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles