26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Waziri Mkuu aipongeza halmashauri Ruangwa

Na MWANDISHI WETU-RUANGWA


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba kwa Mkoa wa Lindi mwaka huu.

Pongezi hizo zlizitoa jana mjini hapa katika mkutano wa kuwapongeza walimu wa Wilaya ya Ruangwa na baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu.

Alisema matokeo ya mwaka jana, Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ilishika nafasi ya tano kwa mkoa na taifa ilikuwa nafasi ya 141, ambako kwa mwaka huu imepanda na kuwa nafasi ya kwanza kwa mkoa na taifa kuwa nafasi ya 84.

Kutokana na   matokeo hayo mazuri, Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imetoa zawadi mbalimbali kwa kata tatu bora zilizofanya vizuri, shule 10 bora, walimu ambao wanafunzi wao wamepata daraja A katika masomo mbalimbali wanayofundisha  na wanafunzi 10 bora.

Awali, akizungumza katika hadhara hiyo, mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa aliupongeza uongozi wa Mkoa wa Lindi kwa mikakati waliyoiweka kwa ajili ya kuboresha elimu, ambayo imesababisha kupatikana   matokeo hayo mazuri.

“Nawapongeza kwa sasa mimi kwa taaluma ni mwalimu hivyo nafahamu ili mwanafunzi apate matokeo mazuri ni lazima mwalimu afanye juhudi kubwa zitakazomuwezesha mwanafunzi kufaulu masomo yake,” alisema.

Ofisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Ruangwa, Selemani Mrope alisema kuanzia mwaka 2015 hadi 2017 hali ya ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba haikuwa nzuri kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya utoro.

Mwalimu Mrope alitaja sababu nyingine kuwa ni walimu kutowajibika ipasavyo, ufuatiliaji na usimamizi duni wa taaluma shuleni ambako viongozi wengi wa shule na kata walishindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao na kuwaacha walimu wafanye kazi kwa mazoea.

“Wazazi wengi kukosa kuwajibika ipasavyo katika elimu ya watoto wao na kuona elimu haina maana kwao na kushindwa kuwahimiza watoto kwenda shule na kusababisha utoro huku wengine wakidiriki kuwashawishi watoto wao wafanye vibaya kwenye mitihani yao,”

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles