24.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 18, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mhagama akabidhi vifaa Tiba Kituo cha Afya Liganga

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),  Jenista Mhagama, amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imejipanga kuboresha huduma za afya ili kuokoa vifo vya akina mama na watoto wakati wa uzazi.

Waziri Mhagama alitoa kauli hiyo, Julai 9, 2024, wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika kata ya Liganga, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama (Mb) wa Peramiho, akizungumza na wananchi katika mkutano wake kijijini Liganga.

“Kituo cha Afya Liganga kimepata vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni mia tatu, hivyo kusaidia kuanza kutoa huduma za matibabu na kupunguza adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya,” alisema Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri ameagiza wataalamu kuhakikisha wanaratibu vyema mipango ya kuunganisha kituo hicho na nishati ya umeme ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai.

Waziri Mhagama alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na kuhakikisha zinatoa huduma bora.

Awali, Dk. Rashid Mfaume, Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, alimsifu Waziri Mhagama kwa juhudi zake za kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Peramiho.

“Jitihada za Mbunge kuomba vifaa tiba kwa vituo vya afya na hospitali zimesaidia sana kuboresha huduma za afya katika Jimbo la Peramiho, ambapo kwa mwaka uliopita fedha nyingi zilielekezwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea,” alisema Dk. Mfaume.

Ameongeza kuwa, zoezi la kukabidhi vifaa tiba ni ishara tosha kwamba Kituo cha Afya Liganga kitatoa huduma zote muhimu zinazopaswa kuwepo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles