29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Makamba azindua kamati kituo cha Dk. Salim Ahmed Salim

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , January Makamba amezindua Kamati ya kupitia majukumu na maboresho ya Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dk. Salim Ahmed Salim zamani Chuo cha Diplomasia

Akizungumza leo Machi 20 jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa kamati wa hiyo, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika miaka mitatu ya uongozi wake kwa kuitangaza nchi kidiplomasia pamoja na kuongezeka idadi ya wageni kutoka nje kuja Tanzania

Amesema lengo la kuzinduliwa kamati hiyo ni kufanya mambo mbali mbali ikiwamo kupendekeza mafunzo, mitaala na kuona namna ya kituo kujenga dhima bora ya fikra.

“Kazi kubwa ya kamati hiyo pamoja na mambo mengine ni kutathimini na kuainisha maeneo yanayohitaji maboresho ili kuwa na kituo chenye kukidhi mahitaji ya wadau wake kwa mahitaji ya sasa na kizazi kijacho,” amesema.

Amesema mialiko na mikutano ambayo Rais amealikwa na kushiriki na viongozi wengine wa Serikali duniani katika ziara alizofanya zimekuwa na mchango mkubwa dimplomasia.

“Ukiona kiongozi sauti yake inatafutwa kwenye mambo muhimu ujue yeye mwenyewe na nchi hiyo ina ushawishi inawezekana katika mabadiliko ya tabianchi, masuala ya rasilimali watu , kilimo, na masuala yote makubwa duniani,”amesema Makamba.

Amesema jambo kubwa kama nchi inalitafuta katika diplomasia ni ushawishi, jitihada zinazofanyika ni kuongeza ushawishi ili kuweza kupata misaada ,wawekezaji kuja kuwekeza ,ushawishi ili misimamo na mitazamo kuhusu masuala mbalimbali ibebe uhusika.

Ameeleza kuwa ushahidi wa hivi karibuni Rais alipokuwa Zanzibar viongozi wawili wakubwa wa Afrika Mashariki walikwenda kumuona Dk. Samia na kuzungumza naye kutokana na ushawishi wake na kusikia mawazo yake , kumuomba msaada na kushauriana nae.

Ameongeza kiwango cha uwekezaji mtaji mwaka 2020 iliyowekezwa nchini ulikuwa wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni moja, mwaka 2023 mtaji uliongizwa nchini ulikuwa ni Dola za Marekani bilioni tano, hiyo ni jitihada za Rais Samia kutokana na ushawishi wake wa kuweka sera za kiuchumi, ambazo zinavutia uwekezaji .

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kituo cha Dk. Salim Ahmed Salim, Balozi Khamis Kagasheki amesema ni kweli katika miaka mitatu kuna mambo mengi yaliyofanyika Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na mataifa mengine.

Ameahidi kuwa katika kamati hiyo watajadili na kuona namna ya kufanya kazi zao ili kuwezesha chuo hicho kurudi katika hali yake .

Kamati hiyo ina wajumbe nane ikiongozwa na Mwenyekiti Balozi Khamis Kagasheki .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles