26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI: MAHUSIANO LAPF, SSRA HAYAKO SAWA

NA ELIYA MBONEA

-ARUSHA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, ameiambia Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF kuwa mahusiano kati ya mfuko huo na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) hayako sawa.

Kauli hiyo aliitoa juzi alipokuwa akizundua Bodi mpya ya tano ya LAPF chini ya Mwenyekiti wake, Professa Faustine Bee, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), mjini hapa.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mbali ya kutoa maagizo kwa Bodi na Menejimenti ya LAPF, Simbachawene aliwataka kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na maelekezo ya msimamizi.

“Niwasihi kuzingatia maelekezo ya msimamizi, msiishi nje ya sheria, kanuni, taratibu na utamaduni wa viwango vya mifuko, kufanya vizuri ni jambo moja lakini pia kuzifuata taratibu ni alama nyingine,” alisema Simbachawene.

Katika maagizo yake kwa Bodi mpya na Menejimenti ya LAPF, aliwataka viongozi hao kuwa makini katika usimamizi wa miradi ya uwekezaji ili iwe yenye tija na faida tarajiwa .

Alisema ni vyema LAPF ikaangalia maeneo yenye uwekezaji wenye tija katika uzalishaji wa ajira kwani shida kubwa katika uchumi wa sasa ni tatizo la ajira.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga, alisema kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za uanzishwaji viwanda.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles