27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri afuta bodi Machinga Complex

02-5Asifiwe George na Secilia Alex(A3), Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, ameifuta bodi ya Jengo la Machinga Complex kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yake.

Waziri Simbachawene, alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati mkutano wake na  Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Simbachawene alifikia uamuzi huo, baada ya risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa JWT, Johnson Minja, kuhusu changamoto zinazowakabili ikiwamo ya kukosa maeneo maalumu ya kufanyia biashara zao.

Alisema amebaini umiliki wa jengo hilo hauna tija kwa sababu umeshindwa kuwajali wafanyabiashara wadogo (wamachinga)na badala yake, jengo hilo limekumbatiwa na baadhi ya wanasiasa.

“Jengo hili ni mali ya Serikali  haliwezi kuchezewa,ni aibu kuona wafanyabiashara wadogo wana wanahangaika kutafuta eneo la kufanyia biashara zao, wakati jengo limekaa bila faida yoyote.

“Ninafanya utaratibu wa wafanyabiashara  kuingia katika jengo hili,wataingia bila masharti  na tutaangalia namna watakavyolipa kodi.

“Jengo hili lilijengwa kwa fedha zilizokopwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)Sh bilioni 12.7,jiji lililipa Sh milioni 50 tu,tunaona hii ni hasara kubwa kwa uchumi  wa nchi, ni vyema wafanyabiashara wa soko la Mchikichini wakaacha kuendelea kunyeshewa ili waendelee kufanya shughuli zao ndani ya jengo hilo,”alisema Simbachawene.

Aliwataka wafanyabiashara kuwafichua watendaji wa Serikali wasiokuwa waaminifu katika utendaji kazi wao ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Alizitaka halmashauri kutotoa liseni kwa wafanyabiashara wa nje na kusema atakaoleta maombi yapitie wizarani.

“Ni marufuku halmashauri kutoa leseni kwa wafanyabiashara wa nje, badala yake maombi yote yapitie wizarani ili ifanye uamuzi wa kuzipitisha.

“Tumebaini leseni zinatolewa kwa wageni kama njugu wakati wafanyabiashara hawana mitaji mikubwa, na zile wanazozifanya ni za milioni tatu hadi tano ambazo wananchi wanao uwezo wa kuzifanya, ni vyema tukawapa wananchi fursa ili nchi yetu iendelea kiuchumi.

Alisema kiwango kilichowekwa kwa ajili ya wafanyabiashara wa kigeni ni kidogo, ni vizuri Serikali ikachukua hatua kupandisha kiwango hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema juzi kwamba alifanya ziara ya kukagua taa katika mitaa mbalimbali na kubaini nyingi hazifanyi kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles