30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri aahidi mil. 200/- ujenzi wa wodi ya nje

Na MWANDISHI WETU-DODOMA

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi kutoa Sh milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Waziri Ummy ametoa ahadi hiyo jana wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la mama na mtoto (Maternity Block) katika Hospitali hiyo ili kujionea hali ya utoaji huduma kwa akina mama wajawazito na watoto.

“Ninaahidi kutoa milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la OPD ya kisasa yenye uwezo wa kupokea wagonjwa wengi zaidi tofauti na OPD iliyopo sasa,” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameutaka uongozi wa hospitali hiyo kurekebisha na kufanya maboresho katika baadhi ya maeneo yaliyoonekana kuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuyapa majina majengo yote ya hospitali hiyo ili kuepusha usumbufu kwa wagonjwa pindi wanapotaka kupata huduma katika majengo tofauti.

Aidha, ameutaka uongozi wa hospitali hiyo kujenga ghorofa ambayo itakua maalum kwa ajili ya matibabu ya watoto pekee yenye uwezo wa kulaza watoto wengi sambamba na chumba cha uangalizi maalum kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda  na wale wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Zainab Chaula, alisema wizara itaendelea kushirikiana na uongozi wa hospitali hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali zilizoonekana katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja kuongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kukidhi mahitaji.

 “Naomba niwaahidi tutaongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kuziba mapungufu yanayoonekana, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika hospitali hii inayotegemewa na watu wengi wa Dodoma na kutoka maeneo ya jirani,” alisema Dk. Chaula.

Hata hivyo Dk. Chaula aliwataka watumishi wa Hhospitali hiyo kushirikiana ili waweze kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wanaokwenda hospitalini hapo.

Katika ziara hiyo iliyoenda sambamba na siku ya Afya Duniani imejumuisha viongozi mbalimbali wa Wizara akiwemo Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Edward Mbaga wameondoka na azimio la kufanya maboresho katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa jengo maalum la kupokea wageni mbalimbali wanaokuja Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles