32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

WAZEE WAFURAHIA MATIBABU BURE

Wazee Wilayani Handeni Mkoani Tanga, wamefurahia utaratibu maalumu wa matibabu bure kwa wazee na kuishukuru serikali kwa kuwatengea mfumo huo.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika Kata ya Kabuku waliofika kujionea namna utaratibu huo unavyofanya kazi na namna wazee hao wanavyonufaika nao, wamesema ni mfumo mzuri  unaowafanya wawe na uhakika wa matibabu.

Wamesema zamani wazee walikuwa wanataabika kwa kukosa fedha za kumudu uchangiaji wa gharama za matibabu jambo lililikuwa likiwakwaza kutokana na wengi wao kuwa masikini.

“Tunaomba mtufikishie salamu zetu za shukrani kwa Raisi Magufuli kwani sasa hivi wazee tunapewa kipaumbele tunapofika hospitalini na kupata huduma hiyo bure raisi wetu Mungu amtunze,” amesema Mmmoja wa wazee hao, Ally Salimu.

Aidha wazee hao pia wamepongeza mpango wa elimu bure, ambapo wamesema kwa sasa wana uhakika wa kuwaandikisha shule wajukuu zao na bila kadhia ya ya michango wala ada.

“Hata mpango wa elimu bure pia umetunufaisha kwani kwa sasa hata sisi masikini watoto wetu na wajukuu wana uhakika wa kusoma hili ni jambo kubwa sana kwetu,” amebainisha mzee Suphiani Mohamedi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles