23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi washuhudia vipaji vya watoto wao

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Wazazi wa wanafunzi wa shule ya chekechea ya Busy Bees wamefurahishwa na vipaji vilivyooneshwa na watoto wao wakati waliposhindana katika michezo mbalimbali ikiwamo soka.

Wanafunzi hao wameshiriki michezo hiyo leo Juni Mosi, 2024 Upanga, jijini Dar es Salaam katika siku maalumu ya michezo ‘Annual Sports Day’ inayoandaliwa na uongozi wa shule hiyo kila mwaka.

Wazazi wa wanafunzi hao wenye umri wa kuanzia miaka 2- 6, walionekana kushangazwa na uwezo wa watoto wao katika kushiriki michezo na kufanya mazoezi.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenzake, Feisal Rashid, amesema wamefurahi kuona watoto wanashiriki michezo kwa pamoja hali inayoleta umoja kwao na wazazi ambao wamekutana.

Amesema kuna faida kubwa kwa watoto hao kuanza kujua umuhimu wa michezo na kufanya mazoezi tangu wakiwa wadogo kwani inawafanya wawe fiti muda wote na kufurahia.

“Michezo ni mizuri inawajenga hata wakiwa wakubwa watakuwa wamezoea mazoezi, Mimi hii ni mara ya pili kushuhudia michezo hii, mwaka jana nilikuwepo na mtoto wangu mmoja lakini mwaka huu ni wawili wameshiriki,”amesema Rashid.

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Busy Bees, Nasreen Murtaza amesema ni kawaida kabla ya kufunga shule mwisho wa muhula kila mwaka wanafanya michezo kwa sababu watoto wanakuwa wanafurahia.

Ameeleza kuwa wameshiriki michezo mbalimbali kwa makundi kutokana na umri wa watoto hao.

“Sisi shule yetu inapromote mtoto kuwa fiti na afya njema, tangu tulipoanzisha shule hii ikiwa ni miaka 16 sasa, tumekuwa tukifanya michezo, watoto wamefurahi na tumewapa zawadi,” ameeleza Nasreen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles