30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WAZAZI NIPENDENI ILIVYOWAFUNDA KINA MAMA  

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


 

picWAKATI serikali ikifanya jitihada za utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Milenia kwa kuboresha huduma mbalimbali za kijamii bado zimekuwapo na changamoto nyingi ambazo zinakwamisha kupiga hatua ya maendeleo kwa kasi kubwa zaidi, hali ambayo inasababisha jamii kukabiliwa na changamoto ya umaskini.

Changamoto hizo zinazidi kuleta adha kwenye jamii baadhi ya kampuni binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali tayari nayo yamebaini kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo si jukumu la Serikali pekee bali kunahitajika mchango pia wa sekta binafsi.

Moja ya kampuni ambayo imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali hususani katika sekta ya afya na elimu ni Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya kijamii ijulikanayo kama Vodacom Tanzania Foundation.

Mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Nzega, Tabu Ramadhan, ambaye anasema yeye ni miongoni mwa Watanzania zaidi ya milioni 1.3

wanaopata taarifa zinazohusiana na afya ya uzazi na malezi ya watoto wachanga kupitia simu zao za mkononi kupitia huduma ya Wazazi Nipendeni ya Wizara ya Afya na wadau wengine kwa kushirikiana na kampuni  yanayotoa huduma za simu nchini ikiwamo Vodacom ambayo inaongoza kwa kuwa na mtandao mkubwa.

“Huduma hii ya Wazazi Nipendeni inatuwezesha Watazania wengi hususani akina mama kupata taarifa zinazohusiana na uzazi kwa urahisi na kwa wakati wowote na huu ni uthibitisho kuwa simu za mkononi si kifaa cha kutumia kuongea tu bali zina matumizi ya ziada ya kuleta manufaa kwa jamii.

“… kama ambayo ujumbe za ufya ya uzazi huwafikia wengi kwa njia hii ya mtandao wa simu za mkononi,” anasema Tabu.

Anasema huduma hiyo maarufu kama Healthy Pregnancy Healthy Baby hivi sasa inatumiwa na idadi kubwa ya Watanzania na kwa kiasi kikubwa imesaidia kupunguza idadi ya vifo vya watoto wanaozaliwa nchini ambapo wazazi hupokea jumbe za maneno kupitia simu zao zenye taarifa za maelekezo kuhusiana na ujauzito na utunzaji wa watoto wachanga bure.

Pamoja na hali hiyo Wazazi Nipendeni imewezesha Watanzania wengi hususani akina mama kupata taarifa zinazohusiana na uzazi kwa urahisi na kwa wakati wowote na huu ni uthibitisho kuwa simu za mkononi si kifaa cha kutumia kuongea tu bali zina matumizi ya ziada ya kuleta manufaa kwa jamii.

Rossalyn Mworia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mawailiano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, anasema; “Vodacom Tanzania Foundation tangu ianzishwe imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye jamii zinazosababishwa kushindwa kufikia malengo endelevu ya milenia hususani katika sekta ya afya na elimu,” anasema.

Anasema moja ya lengo la Milenia namba sita (Millenium Development Goal No. 6) linaelekeza kuzuia na kupambana na maradhi mbalimbali hivyo Vodacom itaendelea kutumia mtandao wake ulioenea nchini kote kuhakikisha unafanya maisha ya Watanzania kuwa murua kwa kupata taarifa za kiafya na kutumika kurahisisha huduma mbalimbali za matibabu.

Anasema mbali na huduma hii Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inatekeleza mradi wa Moyo ambao kwa hivi sasa umeingia katika awamu ya pili na umelata mabadiliko chanya kwenye  jamii.

“Mradi wa Moyo awamu ya kwanza umewezesha wanawake zaidi ya 1,000 kupata matibabu ya bure ya ugonjwa wa Fistula ambapo waliwezeshwa kupatiwa usafiri wa bure kutoka makwao, kupata matibabu ya bure katika hospitali ya CCBRT, kupatiwa maarifa ya kujitegemea katika kituo cha Mabinti na kulipiwa nauli ya kurejea makwao,” anasema Mworia.

Kuhusu  mradi wa moyo awamu ya pili uliozinduliwa mwaka huu katika Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza, umelenga pia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga ambapo wanawezeshwa kupatiwa huduma ya usafiri wa kuwawahisha katika vituo vya afya pindi wakaribiapo  kujifungua ambapo matarajia ya mradi ni kuokoa maisha ya wanawake 225 na watoto wachanga kila mwezi.

Anasema taasisi ya Vodacom Tanzania imejikita katika mapambano ya saratani ya mlango wa kizazi ambapo inaendesha mradi wa kuwasafirisha wanawake wahanga wa saratani kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam, ambapo hadi sasa zaidi ya wanawake 175 wamenufaika

“Uwezeshaji huu unaendelea kupata mafanikio na utekelezaji wake kuwa rahisi kupitia huduma ya malipo ya M-Pesa ya Vodacom ambayo matumizi yake yanazidi kurahisha na kuboresha maisha ya Watanzania wengi,” anasema.

Miradi mingine ya afya ya Vodacom Tanzania Foundation ambayo imeleta faraja kwenye jamii Mworia aliitaja kuwa ni kuwezesha kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa wakunga wa jadi ambapo wakunga wa jadi zaidi ya 500 wamenufaika, elimu ya afya na uzazi kwa wasichana mkoani Mtwara kupitia mradi wa Hakuna Wasichoweza.

Anasema mradi huu umenufaisha wasichana zaidi ya 10,200 na huduma ya Simu Dokta ambayo inawezesha wateja wa Vodacom kupata ushauri wa kiafya kutoka kwa madaktari bingwa kupitia simu zao za mkononi.

“Changamoto zinazowakabili Watanzania ni za kwetu pia kwa kuwa miongoni mwao kuna wateja wetu,”abasema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles