24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wawili wauawa mapigano ya wafugaji na wakulima Handeni

handeni

Na SUSSAN UHINGA,

TANGA

WATU wawili wameuawa na wengine nane wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, kutokana na kuzuka kwa mapigano baina ya wakulima na wafugaji wilayani Handeni.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, David Mnyambunga, ni kwamba  matukio hayo yametokea katika  Wilaya ya Handeni na wilayani Kilindi.

Mnyambunga akieleza tukio la mauaji ya watu wawili alisema lilitokea Novemba 16, saa 11:30 jioni katika kitongoji cha Tengwe, Kijiji cha Manga, wilayani Handeni, baada ya kuzuka mapigano yawakulima na wafugaji.

Alisema mapigano hayo yalitokana na wafugaji jamii ya Wamang’atikutoka Kijiji cha Ng’andu mkoani Pwani kuingiza mifugo yao kwenyemashamba ya wakulima wa maeneo hayo, jambo lililosababisha  uvunjifu waamani.

Aliwataja  marehemu kuwa ni mfugaji  wa jamii hiyo, PapalanKimbini (19) aliyepigwa risasi na katika vurugu hizo na mkulima YassinJoseph aliuawa kwa kuchomwa mkuki mbavuni.

Alielezea kuwa, katika mapigano hayo waliyozimwa na polisi, watu wanane wanashikiliwa kutokana na vurugu hizo na kwamba hali katika maeneo hayo imetengemaa na watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, akizungumza kwanjia ya simu na MTANZANIA alisema vurugu hizo zimesababisha uharibifumkubwa wa mali na kupelekea vifo vya watu 2.

Amesema mpaka sasa hali ya amani ni shwari katika maeneo hayo na kwamba viongozi wa pande zote mbili, kwa maana ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyona Handeni watakutana ili kuweka mikakati ya ulinzi katika mipaka ya vijijivinavyounganisha Mkoa wa Pwani na Tanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles