23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wawili mbaroni kwa kujifanya usalama wa Taifa

Na Yohana Paul, Mwanza

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu wawili waliokuwa wakijitambulisha kwa watu mbalimbali kuwa wao ni watumishi wa Serikali Idara ya usalama wa taifa kitengo cha Afisa kipenyo.

Akitoa taarifa hiyo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema watuhumiwa hao walikamatwa desemba 5 mwaka huu maeneo ya Kamanga, wilayani Sengerema mkoani hapa.

Kamanda Muliro aliwataja watuhumiwa hao ni Severine Edward (32) mkazi wa Kishiri ambaye alikutwa na kitambulisho kilichoandikwa, Severine Edward Mayunga, Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Idara ya Usalama wa Taifa, Kitengo cha Kikosi Maalumu code 82863, nafasi under cover na mwingine ni, Abel Shiwa (46) mkazi wa Kishiri.

Baada ya mahojiano ya kina watuhumiwa wote wamekiri kuhusika na makosa ya utapeli kwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Katika tukio jingine Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa, Hamis Omar (19) mkazi wa Nyasaka Msumbiji kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Vicent Renatus (19) mwanafunzi wa kidato cha pili, shule ya sekondari Katunguru na mkazi wa mtaa wa Msumbiji ambaye alikutwa amefariki na mwili wake ukiwa na majeraha shingo huku kukiwa kumeporwa vitu vya ndani ikiwemo TV na Radio (Sub-Woofer).

Baada ya kuhojiwa kwa kina mtuhumiwa alikiri kuhusika na mauaji ya mwanafunzi huyo naaliwaonyesha askari vitu vilivyoporwa kwa marehemu na kwenda kuviuza kwa Erasto Jackson (22) mkazi wa kitangiri ambaye  naye amekamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma za mhalifu sugu wa kupokea mali za wizi.

Kamanda Muliro pia amethibitisha jeshi la polisi limemkamata na kumuhoji aksari wa jeshi la wananchi Tanzania MT.85507 CPL Silvanus Silvester kwa kosa la kumpiga mateke na kichwa mwamuzi wa Mpira wa miguu, Fadhili Maka (33) na kuharibu kamera ya mwandishi wa habari aina ya Canon mali ya, Abdallah Chausiku (27) katika mchezo wa ligi daraja la kwanza kati ya timu ya Pamba na Rhino Rangers ya Mkoani Tabora  ambapo upelelezi wa shauri hilo bado unakamilishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles