32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wavuvi Kilwa waanzisha ushirika

NA HADIJA OMARY-LINDI

WAVUVI katika Mji mdogo wa Kilwa Kivinje Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, wameunda chama chao cha msingi (Amcos), ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Uvuvi na Mifugo alilolitoa hivi karibuni la kuwataka kuunda ushirika ili waweze kutambulika kisheria. 

Kuundwa kwa ushirika huo sasa kutatoa fursa kwa wavuvi wilayani humo kuanza kunufaika na ruzuku mbalimbali zinazotolewa na Serikali kuendeleza shughuli za uvuvi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hati ya kuandikishwa kwenye ushirika kwa wavuvi hao, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai, aliwataka wavuvi katika maeneo mbalimbali wilayani humo kujiandikisha na kujisajili kwenye ushirika ili kuwa katika mfumo rasmi ambao utawatambulisha kwa umoja.

Alisema miongoni mwa manufaa watakayopata ni mitaji ya kuongeza nguvu katika shughuli zao za uvuvi kama vile mashine, nyavu, teknolojia na mikopo mingine ambayo itawawezesha kukuza shughuli zao.

“Rai yangu hadi sasa Serikali imeshatoa zaidi ya mashine 79 za uvuvi ambapo katika mashine hizo wenzetu Mkoa wa Pwani wameshachukua 49 kupitia vikundi kama hivi vya ushirika, sisi bado mambo hayajakuwa vizuri, nawashauri  wavuvi wenzangu kusudi tuende vizuri katika sekta yetu, hakuna namna nyingine zaidi ya kuwa na vyama vya ushirika vya msingi ili tuweze kutambulika.

“Ukweli ni kwamba  bila kuwa katika vikundi vya ushirika kama hivi kwa kweli tutaendelea kuwa katika uvuvi mdogo ambao hauna tija kwetu na tutakuwa hakuna wa kumlaumu, hivyo ni vyema kujiunga kwenye ushirika ili Serikali iweze kuwaongezea nguvu katika umoja wenu,” alisema Ngubiagai.

Mwenyekiti wa chama hicho, Nasri omari, pamoja na kuishukuru Serikali kwa kuwaunganisha, pia alieleza mikakati ya chama chao ni kuendelea kudhibiti uvuvi haramu unaoendelea katika maeneo yao unaofanywa na baadhi ya wavuvi wasio waaminifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles