27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Wauza Shisha wasalimu amri

Shisha
Shisha

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

WAFANYABIASHARA wa Shisha wamesalimu amri kwa kuacha kuuza bidhaa hiyo baada ya Serikali kuwataka kufanya hivyo ndani ya siku saba kuanzia Julai mosi mwaka huu.

Hayo yalibainishwa   na wafanyabiashara hao  Dar es Salaam jana walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu suala hilo.

“Tunaheshimu kauli ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kupiga marufuku uuzaji wa Shisha.

“Tunaunga mkono uamuzi wa Serikali, kuanzia Julai 4 mwaka huu tulifuata maagizo ya Waziri Mkuu, Majaliwa na Mkuu wa Mkoa Makonda na kufunga biashara ya shisha,” alisema Saphia Said kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake.

Saphia alisema walifahamishwa biashara hiyo inasababisha madhara mbalimbali ukiwamo ugonjwa wa saratani, moyo, ngozi, wajawazito kujifungua watoto wenye uzito mdogo au kabla ya muda.

“Sisi kama kundi la wamiliki, tunapenda kupanua ushirikiano wetu kwa serikali kwa kufunga biashara zetu kwa matumaini kwamba tutapata fursa ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda baada ya sikukuu ya Eid,” alisema.

Alisema lengo la kuomba kukutana na mkuu huyo wa mkoa, ni  kujadili njia tofauti za kutengeneza mazingira mazuri zaidi ya kuendesha biashara yao.

Wafanyabiashara hao waliomba baada ya siku saba kuisha za kufunga   biashara hiyo, waweze kukutana na Makonda kujadili suala hilo kwa undani  lakini kwa sasa ni jukumu lao kutii amri ya serikali na siyo kukoso, alisemaa.

Alisema wanatarajia kujadiliana   Makonda ili kukubaliana ikiwezekana kuwekwa sheria  kuendesha biashara kwa misingi na taratibu kama zilivyo nyingine.

Mfanyabiashara, Jibril Mohamed, alisema   wakati wanaanza biashara hiyo walikuwa wanafuata taratibu za kawaida za kusajili biashara kama zilivyo nyingine.

Alisema kwa vile wameelezwa madhara ya Shisha,  wanafuata agizo la serikali la kuacha  biashara hiyo.

Hata hivyo, alisema kwa sasa hawawezi kusema hasara watakayoipata kwa kuwa ni mapema mno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles