25.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

WAUGUZI WALALAMIKA WATENDAJI SERIKALINI KUWANYANYASA

Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Paul Magesa akizungumza na waandishi wa habari
Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Paul Magesa akizungumza na waandishi wa habari

Na ASHA BANI – Dar es Salaam

CHAMA cha Wauguzi Tanzania (Tanna) kimelalamikia hatua ya baadhi ya viongozi serikalini kutofuata utaratibu wa kushughulikia matatizo ya wauguzi, ikiwamo kutolihusisha Baraza la Wauguzi na Ukunga lenye mamlaka hayo kisheria.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Rais wa Tanna, Paul Magesa, huku akitoa mifano ya wauguzi waliokumbwa na kadhia hiyo ikiwa ni mwendelezo wa vitendo vya wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji serikalini kuwachukulia hatua watumishi wa umma kutokana na madai ya kufanya makosa.

Magesa alitoa mfano wa kilichotokea Mwanza katika Hospitali ya Sekou Toure kwa kile alichokiita muuguzi alipewa adhabu kutokana na mambo ya kibinafsi  na kuliita kuwa ni tatizo.

Aliitaja hospitali nyingine kuwa ni ya Wilaya ya Chunya ambako muuguzi aliyekuwa anatoka zamu usiku, aliwekwa ndani saa 48 bila kupewa nafasi ya kutoa maelezo kisa tu mama mwenye mtoto kulalamika.

“Muuguzi huyu pia hakuwa na makosa ya kitaaluma kama ilivyokuwa imedhaniwa awali na familia ya mgonjwa, jambo linalowavunja moyo wauguzi, inauma na inaumiza sana.

“Pia Mkuu wa Mkoa wa Iringa tulishuhudia akimtisha muuguzi kumfukuza kazi, kwamba kamjibu vibaya na hatimaye wamemshusha ngazi ya mshahara baada ya kumrubuni akubali kuwa alikosea,’’ alisema.

Magesa alisema katika Hospitali ya Rubya, wauguzi walipewa adhabu ya kulima shamba ekari mbili kwa siku nne wakiwa ndani ya sare za kazi na kufutiwa siku nane za mapumziko kwa mwezi nzima.

“Huu ni udhalilishaji wa taaluma kwa hali ya juu na unyanyasaji uliopitiliza,’’ alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles