29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wauguzi, wakunga wakumbushwa miongozo ya utumishi wa umma

Na AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

WAUGUZI na wakunga wamekumbushwa kufuata taratibu na miongozo ya utumishi wa umma na kuzingatia matumizi sahihi ya simu kwa kufuatilia vitu vya msingi na vyenye tija kwa taaluma yao na taifa.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ziada Sellah wakati akizungumza na wauguzi na wakunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila.

Alisema teknolojia inakua kwa kasi, ni wazi kuwa mambo mengi yanabadilika, hivyo wauguzi na wakunga hawana budi kujiendeleza zaidi ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

“Nawashauri muongeze taaluma zaidi ili kuinua kiwango cha huduma za uuguzi na ukunga pamoja na kufanya tafiti ambazo zitaweza kutangaza taaluma yetu na kuonyesha kazi zinazofanywa na wauguzi, hasa ikizingatiwa asilimia 80 ya huduma zinazotolewa hospitalini wauguzi na wakunga wana mchango mkubwa.

“Ninapenda kuwasihi mtumie simu kwa kujiongezea maarifa, ikiwemo kutangaza shughuli za uuguzi na ukunga mnazozifanya ili kuleta matokeo chanya ili jamii iendelee kuthamini na kutambua mchango wenu,’’ alisema Ziada.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza muuguzi wa Muhimbili-Mloganzila, Wilson Fungameza kwa kutengeneza mashine rahisi (CPAP), ambayo inamsaidia kupumua mtoto mwenye matatizo ya upumuaji.

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk. Julieth Magandi, alisema huduma za kiuguzi zimeendelea kuimarika katika Hospitali ya Mloganzila hatua ambayo inaongeza idadi ya wagonjwa.

“Tunahudumia wagonjwa takribani 750 kwa siku, idadi hii inajumuisha wagonjwa wa ndani na wa nje,’’ alisema Dk. Magandi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles