25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

NBS: Serikali pekee inatumia takwimu zetu

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

TANZANIA imeungana na nchi zingine kuadhimisha siku ya takwimu duniani, huku Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikikiri kukabiliwa na changamoto ya  takwimu zake   kutumiwa  na Serikali pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana wakati wa maadhimisho hayo, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk. Albina Chuwa alisema ofisi yake imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya  takwimu wanazozizalisha kutumiwa  na  Serikali pekee.

“Dhana nzima ya matumizi ya utumiaji wa takwimu tunazozalisha hicho ndicho kitu ambacho tunakipigania. Tuna dhana kichwani kwamba takwimu zinazozalishwa ni za Serikali, hapana takwimu ni mali ya umma, tusiiachie Serikali peke yake ikatumia takwimu, zitumike na kila mtu.

“Changamoto kubwa ni matumizi ya takwimu kwa wadau kuiiachia Serikali, maendeleo hayapangwi na mtu mmoja, maendeleo ni kwa kila mtu, basi watu wote tutumie takwimu,” alisema Dk. Chuwa.

Alitolea mfano  katika familia vitu vinapoisha ni lazima takwimu zitumike katika kununua vitu.

“Nitoe mfano katika maisha ya kila siku unapotoka pale nyumbani unapoanza kusema unaenda sokoni, unajua ni lazima uchukue takwimu nini kimeisha; nyanya, vitunguu, mchele na utanunua kilo ngapi na unaangalia nyumbani una watu wangapi.

“Serikali yetu unavyoiona asilimia 100 ya takwimu tunazozizalisha zinatumika na Serikali, sisi watu wengi wakitumia zaidi na zaidi tunafurahi kwa sababu maendeleo hayaletwi na Serikali peke yake, yanaletwa na watu wote,” alisema Dk. Chuwa.

Alisema maadhimisho ya mwaka huu ni ya tatu kufanyika chini ya kaulimbiu ya kuiunganisha dunia kwa takwimu tunazoziamini.

Dk. Chuwa alisema kwa upande wa Tanzania, tangu kupitishwa kwa azimio hilo mwaka 2015 imeendelea kuchukua hatua mbalimbali  za kuendeleza na kuimarisha mifumo ya takwimu rasmi.

“Wito wangu kwa umma na wadau wote kutumia takwimu katika kupanga mipango ya maendeleo  kwani takwimu ni muhimu katika kupanga maendeleo ya watu,” alisema Dk. Chuwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles