TUNU NASSORO
WAUGUZI wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) wamekumbushwa kuzingatia sheria na kanuni wakati wa utoaji huduma kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.
Akizungumza baada ya kutembelea hospitalini hapo juzi, Mwakilishi wa Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC), Happy Masenga, alisema wauguzi wanatakiwa kuzingatia maadili ya taaluma yao.
Alisema kwa kuzingatia Sheria ya Uuguzi ya Mwaka 2010 walifika hospitalini hapo kujiridhisha kama huduma zinazotolewa zinakidhi viwango.
“Tumetembelea wodini kuangalia kama utoaji wa huduma unazingatia sheria na kanuni za uuguzi ambako tumeridhishwa na hali tuliyoiona,” alisema Happy.
Alisema pia wameangalia utoaji mafunzo ya kujiendeleza kazini jambo ambalo amekiri kutekelezwa na MOI.
“Tunasimamia kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa ufasaha kulingana na taaluma,” alisema Happy.
Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi wa MOI, Fidelis Minja alisema pamoja na kuwapo changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitanda vyenye magurudumu, wauguzi hospitalini hapo wameendelea kutoa huduma bora.
“Pamoja na kukosa baadhi ya vifaa ikiwa ni pamoja na vitanda vvyenye magurudumu tumeendelea kutoa huduma bora hasa kwa wagonjwa wa ubongo wenye mahitaji ya vitanda hivyo,” alisema Minja. Alisema wauguzi wanatakiwa kutoa huduma wakiwa kwenye sare, ujuzi na uwezo wa kutoa