25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wauguzi JKCI wakumbushwakuzingatia sheria

TUNU NASSORO

WAUGUZI wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) wamekumbushwa kuzingatia sheria na kanuni wakati wa utoaji huduma kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

Akizungumza baada ya kutembelea hospitalini hapo juzi, Mwakilishi wa Msajili wa  Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC), Happy Masenga, alisema wauguzi wanatakiwa kuzingatia maadili ya taaluma yao.

Alisema kwa kuzingatia Sheria ya Uuguzi ya Mwaka 2010 walifika hospitalini hapo kujiridhisha kama huduma zinazotolewa zinakidhi viwango.

“Tumetembelea wodini kuangalia kama utoaji wa huduma unazingatia sheria na kanuni za uuguzi ambako tumeridhishwa na hali tuliyoiona,” alisema Happy.

Alisema pia wameangalia utoaji mafunzo ya kujiendeleza kazini jambo ambalo amekiri kutekelezwa  na MOI.

“Tunasimamia kuhakikisha   wananchi wanapata huduma bora na kwa ufasaha kulingana na taaluma,” alisema Happy.

  Kaimu Mkurugenzi wa Uuguzi wa MOI, Fidelis Minja alisema pamoja na kuwapo   changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitanda vyenye magurudumu,   wauguzi hospitalini hapo wameendelea kutoa huduma bora.

“Pamoja na kukosa baadhi ya vifaa ikiwa ni pamoja na vitanda vvyenye magurudumu tumeendelea kutoa huduma bora hasa kwa wagonjwa wa ubongo wenye mahitaji ya vitanda hivyo,” alisema Minja. Alisema wauguzi wanatakiwa kutoa huduma wakiwa  kwenye sare, ujuzi na uwezo wa kutoa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles