24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi mahakama kuu Tabora kusaidia yatima

Na Allan Vicent, Tabora

Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora wamejipanga kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo nchini kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa misaada ya kijamii kwa Watoto yatima na Wazee wasiojiweza.

Hayo yamebainishwa jana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Amour Said Khamis alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo mbalimbali vya habari Mkoani hapa.

Alisema kuwa katika maadhimisho hayo yanayotarajiwa kuanza Januari 23 hadi 29, mwaka huu na kilele chake kuwa Februari 1, watumishi wote wa Mahakama watapata fursa ya kutembelea magereza yote na vituo vya kulelea watoto yatima na wenye albinism na wazee wasiojiweza katika wilaya za Igunga na Urambo.

Mbali na kutoa misaada ya kijamii aliongeza kuwa watashiriki zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya akinamama wanapoenda kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo-Kitete na kusaidia watu wote wenye uhitaji huo.

Alisema kwamba mahakama aina jukumu kubwa la kuhakikisha jamii inaishi kwa usalama na usawa ili kujenga amani na mshikamano mkubwa kati ya wadau mbalimbali na mahakama.

“Mahakama iko karibu zaidi na wananchi, ndio maana katika maadhimisho haya tutatoa misaada ya kijamii, elimu na huduma mbalimbali za msaada wa kisheria ili kusaidia wananchi waliokosa haki zao,” alisema.

Jaji Mfawidhi alibainisha kuwa katika maadhimisho hayo yanayoenda sambamba na wiki ya kisheria wamejipanga kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria na utoaji haki kupitia vyombo vya habari, kufanya mihadhara kwenye shule za msingi, sekondari, vyuo na nyumba za Ibada.

Alitaja kauli mbiu ya mwaka huu kuwa ni ‘Miaka 100 ya Mahakama Kuu, Mchango wa Mahakama katika kujenga nchi inayozingatia Uhuru , Haki , Udugu , Amani na Ustawi wa wananchi 1920-2021’.

Aidha alitoa wito kwa wakazi wote wa mkoa huo na wilaya zake zote kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo ili kunufaika na elimu ikiwemo huduma za msaada wa kisheria zitakazotolewa bure na Watumishi wa mahakama za Mkoa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles