30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi Housing Investments yaibuka kidedea tuzo za Sabasaba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) imeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya pili katika tuzo za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), zilizotolewa Julai 13, 2022, katika viwanja wya Maonesho Sabasaba, jijini Dar es Salaam kwenye maadhimisho ya maonesho hayo.

Cheti cha Mshindi wa pili kilichokabidhiwa kwa WHI.

Tuzo hizo zilizoratibiwa na TANTRADE na kukabidhiwa na Makamu wa Rais Dk. Phillip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maonesho hayo Julai 13, 2022 jijini Dar es Salaam

Aidha, Watumishi Housing Investments (WHI) iliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya pili katika kundi la Mtoa huduma bora za makazi (Real Estate) wa mwaka katika maonesho hayo.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dk. Fred Msemwa ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kutambua mchango wa WHI katika kutoa makazi bora nchini hasa kwa wafanyakazi.

“Sisi WHI tunaishukuru Tantrade kwa kutupatia tuzo hii kwani itaendelea kuchochea na kuongeza hamasa kwa WHI kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi nyakati zote.

“Lengo la WHI ni kuona Watanzania wakipata makazi bora na ya kisasa kwa bei nafuu ndiyo sababu tumeendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika sehemu tofauti za Jiji la Dar es Salaam na kwingine nchini,” amesema Dk. Msemwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dk. Fred Msemwa(kulia), akisikiliza na kuhudumia wateja wanaoendelea kutembelea banda letu katika maonesho ya 46 ya sabasaba.

Maonesho hay ya 46 yaliyokuwa na Kauli Mbiu ya “Tanzania ni sehemu sahihi kwa Biashara na Uwekezaji” yalianza rasmi Juni 28, 2022 na kufungwa Julai 13, 2022

TANTRADE huwa na utaratibu wa kuandaa tuzo hizi kila mwaka kwa kutambua mchango wa Taasisi/Mashirika/Kampuni katika kutoa huduma kwa wananchi hususani katika kipindi cha maonesho ya Sabasaba.

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda(kushoto) akipata maelezo ya miradi inayotekelezwa na WHI kutoka kwa Meneja Masoko au Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Raphael Mwabuponde, alipotembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya Sabasaba.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberata Mulamula amefanikiwa kutembelea Banda la Watumishi Housing Investments lililopo katika viwanja vya sabasaba ndani ya ukumbi wa Karume na kupatiwa maelezo ya kina juu ya upatikanaji wa Nyumba Bora kwa Bei nafuu kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa sekta binafsi, wafanyabiashara na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles