29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kili Challenge yapandisha watu 52 Mlima Kilimanjaro kwa ajili Mwitikio wa UKIMWI nchini

Na Nadhifa Omary, Kilimanjaro

Washiriki 52 wamepanda Mlima Kilimanjaro kupitia program ya Kili challenge 2022 inayoratiwa na Mgodi wa Geita Gold mine, kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa lengo la kukusanya fedha za kudhibiti UKIMWI Nchini.

Akizungumza wakati wa kuaga wapanda Mlima hao waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene, amesema uzalendo upo wa aina tofauti hata hili la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa nia ya kukusanya fedha kwa ajili ya watu wanaoishi na VVU nalo ni suala la kizalendo kwa kuwa mtu anakuwa amejitoa kwa ajili ya watu wengine wenye uhitaji.

“Uzalendo ni upo wa aina tofauti, hawa wenzetu wanaojitoa kupanda mlima hadi kileleni na wanaozunguka mlima kwa kutumia baiskeli wanaonesha aina ya uzalendo, kwani hawa wanajitoa kwa ajili ya watu wengine ambapo fedha zinazopatikana kupitia prigram hii zinasaidia katika mwitikio wa UKIMWI pamoja na kusaidia watu wengine wenye uhitaji

“Niwashukuru GGM kwa hii program kwani inalenga kupunguza athari za kupungua kwa misaada ya wahisani na kuiwezesha nchi kuimarisha uwezo wa ndani kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI,” amesema lisema Simbachawene. 

Aidha, ameongeza kuwa hughuli hiyo ya uzinduzi wa Harambee ya kupanda Mlima Kilimanjaro sambamba na kuwaaga wapanda mlima na waendesha baiskeli kuzunguka Mlima kwa mwaka 2022 kwa ajili ya kupata fedha za kudhibiti VVU na UKIMWI ni mwelekeo mzuri wa kuunga mkono jitihada za kujenga uwezo wa ndani badala ya kutegemea zaidi misaada ya wahisani pekee. 

Waziri ameipongeza  bodi ya Kili Trust kwa kuwa na utaratibu wa kuidhinisha kiasi cha fedha zinazopatikana kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (AIDS TRUST FUND) ulioanzishwa na Serikali kupitia Bunge tangu mwaka 2015,ambapo katika hafla hiyo ATF ilipatiwa hundi ya shilingi milioni 75.

Awali, Dk. Leonard Maboko alisema dhima ya Kilimanjaro Challenge Against HIV AIDS 2022 tangu ilivyoasisiwa mwaka 2002 katika historia ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini ni kushirikisha wadau kuchangia kwa hali na mali mwitikio wa  Taifa dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

Dk. Maboko amefafanua kuwa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ni jambo linalohitaji ushirikiano wa serikali na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi hivyo Katika kipindi cha zaidi ya miongo minne tangu UKIMWI ulipogundulika nchini, serikali ya Tanzania ikishirikiana na wadau katika mwitikio wa kitaifa imekuwa ikiongeza jitihada za kupambana na maambukizo ya ugonjwa huu, hadi hali sasa inaonesha kupatikana kwa mafanikio makubwa katika kuudhibiti kutokana na kuimarika kwa upatikanaji wa huduma mbalimbali za VVU na UKIMWI.

Dk. Maboko amewaomba wadau kuendelea kujitokeza kuchangia Mwitikio wa UKIMWI nchini ili kuendelea kuziba pengo linalopungua kutoka kwa wafadhili na kutimiza dhana ya kujitegemea kwa kutumia raslimali za ndani na kupunguza athari zitokanazo na UKIMWI.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles