Kongo , DRC
Wapiginaji wenye silaha wamewaua takriban watu 19 wakiwemo wanajeshi kumi baada ya kushambulia vijiji viwili mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo siku ya jumamosi muda muda mfupi baada ya Rais Felix Tshisekedi kutangaza kwamba mikoa miwili mashariki mwa nchi hiyo Ituri na Kivu Kaskazini ,imezingirwa .
Ongezeko la mashambulizi ya makundi yaliyojihami na machafuko ya kikabila yamesababisha vifo vya watu Zaidi ya 300 tangu mwanzoni mwa mwaka huu huku wanajeshi wa serikali na walinda amani wa umoja wa mataifa wakijaribu kuleta utulivu mashariki mwa nchi hiyo .
Shambulio la hivi punde limefanyika siku ya jumamosi wakati wapiganaji wenye silaha waliposhambulia vijiji viwili katika mji wa Kivu kaskazini wa Beni, mamlaka za jimbo hilo zimesema
Baadaye siku hiyo imam mwenye ushawishi mkubwa aliuawa kwa kupigwa risasi msikitini mjini Beni alipokuwa akiwaswalisha watu wakati wa jioni . Alitambulika kwa kupinga itikadi kali za kidini kupitia kitu kimoja cha redio katika jimbo hilo.
” Lengo ni kumaliza kabisa ghasia ambazo zimesababisha mauaji ya wananchi katika sehemu hii ya taifa kila siku’ amesema msemaji wa serikali Patrick Muyaya ambaye hakubainisha kitakachofuata baada ya hali hiyo kutangazwa katika mikoa hiyo miwili .
Siku ya ijumaa Polisi katika mji wa Beni waliwatawanya wanafunzi waliokuwa wakifanya maandamano ya kuketi katika ukumbi mmoja wa mji humo kulalamikia ongezeko la hali ya ukosefu wa usalama.
Watu kadhaa walijeruhiwa na wengine kukamatwa kulingana na shahidi mmoja aliyezungumza na shirika la habari la Reuters.