26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Watoto 70 hatarini kukosa upasuaji moyo

Pg-3

NA HADIA KHAMIS, DAR ES SALAAM

ZAIDI ya watoto 70 wenye matatizo ya moyo wako hatarini kukosa huduma ya upasuaji mkubwa wa moyo kutokana na uhaba wa damu unaoikabili Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Maulid Mohammed, alisema watoto hao wanatarajia kufanyiwa upasuaji Septemba 9 hadi 19.

Alisema zaidi ya chupa za damu 300 zinahitajika ili kufanikisha upasuaji huo.

“Upasuaji huo utafanyika kwa kushirikiana na taasisi inayoshughulikia masuala ya watoto ya nchini Marekani (Mendig Kids) ambayo italeta madaktari kutoka Italia, ambao watashirikiana na madaktrai bingwa wa magonjwa ya moyo,” alisema. Mohammed.

Alisema upasuaji mkubwa wa moyo unatumia damu nyingi, hivyo kwa kulitambua hilo, lazima kuwapo kwa damu ya ziada.

“Tunahitaji damu nyingi itakayoweza kutusaidia wakati wa upasuaji wa watoto hawa, damu ndiyo njia pekee itakayoweza kufanikisha kazi hii muhimu,” alisema Mohammed.

Aliwataka watu mbalimbali, zikiwamo taasisi za Serikali, zisizokuwa za Serikali na taasisi za dini kujitokeza ili kuchangia damu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles