26.4 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

WATOTO 67 WA KIKE WAKATALIWA NA WAZAZI WAO


Na TIMOTHY ITEMBE - TARIME

WATOTO 67 wa kike kati ya 2,572 waliokimbilia Kituo cha Msanga kinachopokea na kulea watoto wa kike waliokimbia nyumbani kwao kuogopa kukeketwa, wamekataliwa na wazazi pamoja na walezi wao.

Kutokana na kitendo hicho, kituo hicho kimechukua jukumu la kuwapeleka shule kuanza masomo kwa mwaka huu, huku kikiiomba Serikali kuingilia kati kwa kuwachukulia hatua wazazi na walezi waliokataa kuwapokea watoto hao.

Akizungumza wakati wa kufunga mahafali ya kufunga kambi,  Meneja wa mradi wa Association For Termination of Female Genital Multilation (ATFGM) ulio chini ya kituo hicho, Valerian Mgani, alisema  wamesikitishwa na wazazi na walezi kukataa kuwapokea watoto hao.

Alisema wazazi hao wamewakataa watoto hao kwa sababu walikimbia makazi yao kukwepa kutii mila zao.

“Kama wazazi, walezi na jamii imewakataa watoto hawa sasa tunafanyaje, kituo kimebeba jukumu la kuwapeleka  shuleni kusoma, ikiwamo shule za msingi na sekondari.

“Tangu kuanzishwa kwa kituo hiki mwaka 2008, tumekuwa tukipokea watoto ambao wanakimbia ukatili, ikiwemo ukeketaji na wengine kwa ajili ya kupata elimu juu ya tohara mbadala kutoka wilaya za Serengeti, Tarime, Loliondo na nchi jirani ya Kenya.

“Huwa kuna utaratibu wa mafunzo ya muda katika kambi zetu, tunatenga baadhi ya watoto na kuwapa elimu kwa kuwahusisha wazazi, na kambi zinapomalizika watoto hao hulazimika kurudishwa nyumbani kwao, lakini  baadhi yao wamekataliwa na wazazi wao kwa kile kinachodaiwa kuwa wamekataa mila kwa kukimbia kukeketwa… hadi sasa kuna mabinti 67 waliokataliwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles