29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KENYATTA


Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kutokana na msiba uliopoteza watu 36 kwenye ajali ya barabara iliyotokea Nakuru Eldoret nchini humo.

Katika salamu hizo alizozituma juzi usiku, Rais Magufuli, alisema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa kuhusu ajali hiyo iliyopoteza uhai wa wananchi hao wa Kenya.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kutokea kwa ajali iliyosababisha ndugu zetu takribani 36 kupoteza maisha baada ya basi la abiria kugongana na lori katika barabara ya Nakuru – Eldoret nchini Kenya.

“Msiba huu umesababisha majonzi makubwa si tu kwa ndugu zetu wa Kenya, bali pia kwetu sote wana Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumepoteza wapendwa wetu na nguvu kazi yetu.

“Kwa niaba ya Watanzania wote, nakupa pole sana ndugu yangu Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa msiba huu mkubwa ulioupata, nawapa pole wanafamilia wote waliowapoteza jamaa zao na pia nawapa pole wananchi wote wa Kenya.

“Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, nawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapone haraka na marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina,” alisema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles