Na Ramadhan Hassan, Dodoma
Sheikhe wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu amewaomba Watanzania kuenzi mazuri yote yaliyofanywa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Magufuli huku akimwelezea kwamba alikuwa kiongozi aliyemtanguliza mungu kwa kila jambo.
Pia, amemtakia kila la heri katika utendaji kazi wake Rais mpya Samia Suluhu Hassan huku akidai hana shaka na
Akizungumza jana wakati wa Ibada ya Swala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti wa Gadaffi jjini hapa,,Sheikhe Rajabu ambaye pia ni Kadhi wa Mkoa wa Dodoma amesema watanzania wanatakiwa kuyaenzi yale yote mazuri yaliyofanywa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Dk.Magufuli ikiwemo kumtanguliza mungu kwenye kila jambo.
“Enyi waja wamungu wote tunaelewa aliyekuwa Rais Dk.John Magufuli kila sehemu alipokuwepo alikuwa anapenda sana kumtaja mungu na kumtanguliza mungu wote tulikuwa mashahidi hasa neno niombeeni.
“Ile kusema niombeeni aliyepo mwenye kuombwa ni mungu alimtanguliza sana mungu vikao vyake ilikuwa ni lazima amtaje mungu sote tunafahamu imani yake dhabiti aliyokuwa nayo hata katika Covid, dunia ilitikisika lakini yeye hakutetemeka wala hakutikisika kwanini kwasababu alimtanguliza mungu na alifahamu jambo lolote analeta mungu na hakuna wa kuondoa isipokuwa mungu,”amesema.
Amesema marehemu Magufuli aliwapenda watu hasa maskini ambapo kiu yake kubwa ilikuwa ni wakuona wakifanikiwa katika maisha yao.
“Hakuna aliyemaliza mipango yake ndipo mwenyezimungu akasema kifo kipo mimi na wewe na mwingine swali la kujiuliza tunajiandaaje,tumejiandaaje,Mwenyezimungu anatumbia ‘jinyakulieni zawadi hakuna zawadi bora kama kumcha alllah na kujizuia yale ambayo ametukataza’”amesema.
Amesema kuwa enzi za uhai wa Rais Magufuli alimtanguliza Mungu kwa kila jambo na ndiyo maana aliweza kufanikiwa kwa vitendo,ikiwemo nidhamu kwa watumishi wa umma.
Sheikhe Rajabu amewaomba watanzaia kuendelea kuwa na utulivu katika kipindi hichi kigumu huku akiwasisitizia kuzidi kuliombea Taifa.
“Tutaendelea kufanya maombelezi yetu kwa utulivu kwa sababu atakalo mungu hakuna wa kulizuia mungu kataka kumchukua na sisi tulitaka asiondoke chamsingi sote kwapamoja na kuungana kukuombea Taifa letu na kumuombea Rais mpya Samia,”amesema.
Vilevile,amesema anaimani kubwa na Rais mpya kwani ni mpenda dini ambaye amekuwa kila muda akienda kuswali katika msikiti wa Gadaffi.
“Na yeye ni muumini mwenzetu hatuna shaka na uongozi wake na busara na hekima zake kwa sababu yeye anatokana na marehemu Magufuli katiba imemuona kuwa anafaa kurithi na mara kadhaa alijitambulisha kwamba wao ni pamoja na waliofunzwa na Magufuli.
“Tumuombee mungu amlinde ampe afya,umri mrefu na ajalie yale yote aliyaazimia kuyatekeleza marehemu Magufuli ayamalizie na awe ni suluhisho la watanzania kama jina lake lilivyo hatuna cha kusema wamefanya mengi mazuri,”amesema.